104. Twasoma, ni njema sana

 1. Twasoma, ni njema sana

Mbinguni, kwa Bwana;
Twasoma, dhambi hapana,
Mbinguni kwa Bwana;
Malaika wema wako,
Vinanda vizuri viko,
Na majumba tele yako,
Mbinguni kwa Bwana.

2. Siku zote ni mchana,
Ni nchi ya raha;
Wala machozi hapana,
Ni nchi ya raha;
Walioko wanuona
Uso wa Mwokozi, tena
Jua jingine hapana,
Ni nchi ya raha.

3. Nyama na vitu viovu
Havimo kabisa;
Kifo nacho, na ubovu,
Havimo kabisa.
Ni watakatifu wote,
Wameoshwa dhambi zote;
Wasiosafiwa wote
Hawamo kabisa.

4. Tuna dhambi, pia sote,
Mwokozi akafa;
Kwake tutaoshwa zote,
Mwokozi akafa;
Kwake twapata wokovu,
Tutawona utukufu;
Mbinguni tutamsifu;
Mwokozi akafa.

5. Baba, mama, ndugu zetu,
Twendeni kwa Bwana;
Huku chini sio kwetu,
Twendeni kwa Bwana;
Tusishikwe na dunia,
Na dhambi kutulemea;
Tutupe vya chini pia,
Twendeni kwa Bwana.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu