108. Twenenda Sayuni

 1. Mpendao Bwana

Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha
Wa ibada yenu.

 Twenenda Sayuni,
 Mji mzuri Sayuni;
 Twenenda juu Sayuni
 Ni maskani ya Mungu.
          
2. Wasiimbe wao
wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio
waimbao chini.

3. Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika Mbinguni
Kwenye utukufu.

4. Tutakapo mwona
Masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima,
Anasa halisi.

5. Tupaaze sauti,
Na fute machozi,
Twenenda kwa Imanweli
Naye ni Mwokozi.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu