111. Neno Lako Bwana

 1. Neno lako, Bwana,

Ni imara sana;
Lilo latwongoza,
Lilo latufunza.

2. Adui wabaya
Wakikaribia,
Neno lake Bwana
Ni ulinzi sana.

3. Siku za dhoruba
Soma ukiomba;
Neno lake Bwana
Msaada sana.

4. Ukiliamini,
Hwenda na amani;
Una na furaha
Neno ni siraha.

5. Ni furaha kweli,
Na wingi wa mali,
Neno lake Bwana
Kwa wasiokana

6. Neno la rehema,
Tukali wazima;
Faraja I papo,
Tufarikanapo.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu