112. Nilikupa Wewe Maisha Yangu

 1. Nilikupa wewe

Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

2. Nilikupa miaka
Yangu duniani
Upate inuka,
Kuishi Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini:

3. Niliacha nuru
Za Baba, Mbinguni,
Kwingia taabu
Za ulimwenguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

4. Niliteswa sana,
Mateso kifoni,
Usije yaona
Hayo ya motoni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

5. Nimekuletea
Huku duniani
Upendo na afya
Zatoka Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

6. Nipe siku zako,
Udumu mwangani;
Na taabu yako,
Wingie rahani
Nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu