113. Ni Mfalme wa mapenzi

 1. Ni Mfalme wa mapenzi

Ndiye anichungaye,
Sipungukiwi, hawezi.
Kunipoteza yeye.

2. Kando ya mji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisho mema
Daima hunilaza.

3. Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu,
Naye huniandamia,
Hunirudisha kwangu.

4. Uvulini mwa mauti,
Siachi hatari kamwe,
Wewe Bwana huniachi,
Mwokozi wangu wewe.

5. Waniandikia meza
Neema kwako tele.
Kwa wewe, yote naweza.
Na msalaba mbele.

6. Kamwe hautapungua
Uule wema wako;
Mwisho, atanichukua,
Juu, niimbe kwako.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu