119. Si damu ya nyama
1. Si damu ya nyama
iliyomwagika,
iwezayo kuondoa
dhambi za wakosa.
2. Yeye Bwana Yesu
sadaka ya Mungu,
mwenye damu ya thamani,
Ni mwokozi kweli.
3. Kwa imani yangu,
namshika yeye,
naziweka dhambi zangu,
juu ya kichwa chake.
4. Mzigo wa dhambi
sichukui tena,
ameuchukua yeye,
juu ya msalaba.
5. Bwana Yesu ndiye,
mwokozi wa kweli,
tumsifu siku zote,
twapata uhuru.
Comments
Post a Comment