120. Enyi wanadamu

 1. Enyi wanadamu mbona

Sana mwatanga-tanga,
Kama kondoo wanyonge,
Wasio na mchunga?
Yuko mchunga mmoja
Mwenye mapenzi mema;
Haya kutaneni kwake,
Atawachunga vyema.

2. Mungu tunamwona kuwa
Mwenye uwezo wote;
Na nguvu zake zapita
Mawazo yetu yote:
Ni Baba,mapenzi yake
Ni makubwa hakika;
Hatuwezi kuyajua,
Na hayana mpaka.

3. Rehema za Mungu nazo
Zina upana sana;
Kama huo wa bahari,
Mwisho wake hapana;
Haki yake ina mema,
Kwa hayo twashukuru,
Kwetu uko msamaha,
Furaha na uhuru.

4. Mapenzi yake mapana,
Sisi hatuna cheo
Cha kutosha, nao moyo
Una wema upeo;
Ukombozi mwingi mno
Katika damu yake;
Sote twapata furaha,
Kwa maumivu yake.

5. Yesu mkaribieni
Njoni msife myoyo;
Njoni kwake kwa imani,
Mema yake ni hayo;
Heri tuwe kama wana
Tushike neno lake,
Daima atujaza
Tele furaha yake.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu