140. Mahali ni Pazuri
1. Mahali ni pazuri,
ndugu wanapokaa,
/: wakipatana vema,
na wakipendana. :/
2. Kama umande mzuri,
unyweshavyo shamba,
/: vivyo na Mungu wetu,
hubariki ndugu. :/
3. Upendano hujenga,
boma zuri kwao,
/: wakae na amani,
waliookakoka. :/
4. Na ulimwengu wote,
watiwa nuruni,
/: halafu kundi moja,
na mchunga mmoja tu. :/
Comments
Post a Comment