145. Ndoa Yetu Nzima

 1. Ndoa yetu nzima

simika, Yesu!
Usiku na mchana
uwepo kwetu.
Leo tuna raha,
Wewe watupa.
/:Ndoa yetu Bwana
ndiwe Baraka!/:

2. Atoka kijana,
ataka mchumba
siku zinapita
za kupimana.
Leo twapatana
pamoja kukaa
/:Ndoa yetu…:/

3. Vyote hapa chini
vinakaa muda,
vyote vinaoza,
tena vyachakaa.
Pendo la duniani
nalo huchakaa
/:Ndoa yetu…/:

4. Kakaa kwetu Bwana,
kutukagua,
pendo letu sisi
lisichakae:
Hivi na tukae
na baraka tu.
/: Ndoa yetu…:/

5. Kana arusuni
ulialikwa,
walivyoishiwa
ukaongeza,
nasi shida zetu
utazishinda.
/:Ndoa yetu..:/

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu