154. Bariki Yote Yawe Mema

 1. Bariki yote yawe mema,

yote yawe mbaraka.
Watu wa nchi za duniani,
uwajaze utukufu.

  Kaa kwetu, Bwana, bariki.
  Uamini wee ee ndugu
  kweli yake Kristo.
  Jaa utukufu wa Bwana
  siku zako zote.
  /:Vaa Mwokozi ee
  na kweli yake, Haleluya.:/

2. Nyumba za wote zibariki
kwa Jina lako takata.
Ujaze utukufu wako,
nchi zote dunia,
Kaa kwetu, Bwana…

3. Nyosha mkono ubariki,
waliojiunga nawe.
Wakupokee maishani,
watunzwe nawe milele.
Kaa kwetu, Bwana…..

4. Bwana yatunze mambo yote
yaliyo mazuri kwako
Uwape wote wakuombao,
wafanikishe maisha.
Kaa kwetu Bwana….

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu