157. Kijito cha Utakaso

 1. Kijito cha utakaso

ni damu ya Yesu,
Bwana anao uwezo
kunipa wokovu

 Kijito cha utakaso,
 Nizame kuoshwa humo
 Namsifu Bwana kwa hiyo
 Nimepata utakaso

2. Viumbe vipya naona;
damu ina nguvu,
meharibu uovu
ulionidhulumu

3. Naondoka kutembea
nuruni mwa mbingu,
Na moyo safi kabisa
kumpendeza Mungu.

4. Ni neema ya ajabu
kupakwa na damu;
na Bwana Yesu kumjua
Yesu wa Msalaba.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu