46. Twae wangu uzima
1. Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku,
Zikutukuze huku
Tazama! Tazama! Tazama uishi!
Mtazame huyo aliyeangikwa juu.
Hivi sasa upate ishi..
2. Twae mikono nayo
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu.
3. Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.
4. Twae dhanabu pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.
5. Nia itwae, Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako.
6. Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Nniwe wako halisi.
Comments
Post a Comment