55. Nipe Moyo Wenye Sifa


1. Nipe moyo wenye sifa
Sio wa utumwa;
Moyo ulionyunyizwa
Damu ya thamani.

 Mweupe tu, ndiyo mweupe,
 Ukiniosha nitakuwa safi.
          
2. Moyo msikizi, moyo
Wa kunyenyekea,
Moyo utawaliwao
Na Mwokozi pia.

3. Mwenye kutubu, mnyonge,
Sadiki, amini;
Kamwe, kamwe asitengwe
Akaaye ndani.

4. Mpya, mwema na mawazo
Mwingi wa mapenzi
Nawe uwe kielelezo
Moyo wa Mwokozi.

5. Ni uule moyo wako;
Moyo wa huruma
Yesu, natamani kwako
Kukujua vyema.

6. Na ya midomo matunda
Yako, nipe nami;
Amani isiyokoma
Iwe yangu mimi.

7. Nitie yako tabia,
Inishukie juu;
Jina lako nipe pia,
Ndilo la upendo.

8. Ni wa baba utukufu;
Mwana atukuke;
Na roho Mtakatifu
U utatu pweke.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu