58. Mwamba Mwenye iMara


1. Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha!
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.

2. Kwa kazi zote pia,
Sitimizi sharia.
Nijapofanya bidii,
Nikilia nakudhii,
Hayaishi makosa;
Ndiwe wa kuokoa.

3. Sina cha mkononi,
Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike;
Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.

4. Nikungojapo chini,
Nakwenda kaburini;
Nipaapo Mbinguni,
Na kukwona enzini:
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu