63. Ndugu wa kirohoni

 1. Ndugu wa kirohoni

Mliokombolewa,
Tafakarini sana
Yatupasayo.

 Wapenzi wake Yesu
 Tuliokombolewa
 Tujitoe kabisa
 Wengi waponywe.
          
2. Siku itatimia
 Tutakapoulizwa
 Wale wa nyumba zetu
 Na majirani

3. Tujitoeni, ndugu,
Tukahubiri Injili.
Atutumie Roho
kuponya wengi.

4. Wasiokombolewa
Ni wengi vijijini,
Wataokolewaje
Tukiogopa?

5. Bwana alijitoa
Akapotewa mengi,
Ili atuokoe,
Tusiwe waoga.

6. Aliyetununua,
Kwa kuimwaga damu,
Angalieni sana
Msimwepuke.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu