68. Mungu msaada wetu

 1. Mungu msaada wetu

Tangu myaka yote,
Ndiwe tumaini letu
La zamani zote.

2. Kivuli cha kiti chako
Ndiyo ngome yetu.
Watosha mkono wako
Ni ulinzi wetu.

3. Kwanza havijakuwako
Nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako
Twakaa salama.

4. Na myaka elfu ni kama
Siku moja kwako;
Utanilinda daima
Tu wenyeji wako.

5. Binadamu huondoka,
Mwisho hana kitu;
Kama ndoto hutoweka
Ndivyo hali yetu.

6. Ila wewe Mungu wetu
Ndiwe wa kudumu;
Ndiwe bora, ngome yetu
Twakaa dawamu

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu