74. Wachunga walipolinda

 1. Wachunga walipolinda

Kucha nyama zao,
Malaika mtukufu
Alishuka kwao.

2. Wakacha sana wachunga,
Akawatuliza,
“Nawaletea habari
Ya kuwapendeza.”

3. ”Mji ule wa Daudi
Leo amezawa
Mwokozi ni Kristo Bwana,
Ilivyoandikwa”.

4. ”Huyo mwana wa Mbinguni
Ataonekana,
Amelazwa kihorini
Malazi hapana.”

5. Alipokwisha yanena
Malaika hao
Waliimba wimbo huu
Usio na mwisho:

6. ”Enzi ni yake Munju juu,
Na nchi salama,
Kwa watu nao radhi kuu,
Sasa na daima.”

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu