77. Msalabani Pa Mwokozi

 1. Msalabani pa mwokozi,

Hapo niliomba upozi,
Akaniokoa mpenzi,
Mwana wa Mungu.

 Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
 Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
          
2. Chini ya mti msumbufu,
Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.

3. Aliniokoa dhambini,
Ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia mtini,
Mwana wa Mungu.

4. Damu ya Yesu ya thamani,
Huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni,
Mwana wa Mungu.

5. Hicho kijito cha gharama,
Leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima,
Mwana wa Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu