81. Chini ya msalaba

 1. Chini ya msalaba

Nataka simama;
Ndio mwamba safarini,
Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu
Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu
Wakati wa hari.

2. Hapa ni pema sana,
Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana,
Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa
Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa
Ngazi ya Mbinguni.

3. Na Yesu msalabani
Walimkemea,
Alikufa niokoke
Niliyepotea;
Naona ajabu sana
Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda,
Nisiyestahili.

4. Atakayeonana,
Na Yesu Mbinguni,
Njia yake aanzapo
Ni msalabani;
Wokovu upo hapa tu,
Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu
Pamoja na Bwana.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu