82. Sioni Haya Kwa Bwana

 1. Sioni haya kwa Bwana

Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara!

 Msalaba ndio asili ya mema,
 Nikatua mzigo hapo;
 Nina uzima, furaha daima,
 Njoni kafurahini papo.
          
2. Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi,
Alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi.

3. Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.

4. Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu