88. Ndiyo Damu ya Baraka

 1. Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa,

Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.

 Safi kabisa; safi kabisa!
 Nioshe katika damu;
 Takuwa safi kabisa.
          
2. Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.

 Safi kabisa; safi kabisa!
 Ndicho kinitakasacho,
 Nami ni safi kabisa.
          
3. Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa;
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.

  Safi kabisa; safi kabisa!
  Nioshe kwa damu yako,
  Nami ni safi kabisa.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu