89. Kwa Kalvari

 1. Muda mwingi nilipotea,

Sikufahamu msalaba,
Wala aliyenifilia,
Kwa Kalvari.

 Rehema bure na neema,
 Samaha nalo nilipewa,
 Ndipo aliponifungua
 Kwa Kalvari.
          
2. Kwa neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona mimi mwovu,
Nikageuka na kutubu,
Kwa Kalvari.

3. Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye mfalme wa pekee sasa,
Kwa furaha nitamwimbia,
Wa Kalvari.

4. Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema ilishuswa toka juu,
Alitufanyia wokovu
Kwa Kalvari.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu