95. Hivi vita vimekoma

 1. Hivi vita vimekoma,

Vimeshindwa na uzima,
Na asifiwe daima,
Bwana Yesu.

 Aleluya! Aleluya! Aleluya!
          
2. Nguvu za kifo ni hizo,
Ila hazina uwezo,
Ndizo sasa avunjazo,
Bwana Yesu.

3. Siku tatu za huzuni,
Kisha atoka ufuni,
Asifiwe duniani,
Bwana Yesu.

4. Mapingu ameyavunja,
Mbingu amezifungua,
Nasi sasa twamwimbia,
Bwana Yesu.

5. Na ulivyopigwa wewe,
Ni kwamba tufunguliwe,
Milele na usifiwe,
Bwana Yesu.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu