97. Tazameni huyo ndiye

 1. Tazameni huyo ndiye,

Mwenye kushinda vita;
Haya, tumsujudie;
Nyara anazileta;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.

2. Msifuni malaika,
Mtukuzeni sana,
Wote waliookoka
Watamsifu Bwana;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.

3. Walimfanya dhihaka
Zamani wenye shari,
Kwao waliookoka
Ni Bwana wa fahari;
Watu wote msifuni.
Sasa yumo Kitini.

4. Nyimbo nzuri, sikizeni,
Ni nyimbo za sifa kuu,
Za Bwana Yesu kitini,
Kutawazwa, yeye tu;
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu