98. Huyo ndiye! anashuka

 1. Huyo ndiye! anashuka,

Aliyetufilia,
Wengi waliookoka,
Wakimfurahia,
Aleluya!
Yesu aturudia.

2. Sote tutamtazama,
Amekaa kitini,
Nao waliomchoma,
Kumkaza mtini,
Na kilio, wamuone enzini.

3. Alama za kifo chake
Hata sasa anazo
Na waaminifu wake
Wapendezewa nazo.
Alipata,
Kwetu alama hizo.

4. Wokovu utakiwao
Sasa wapatikana,
Na watakatifu hao
Mbinguni wakutana
Kumlaki,
Ndiyo siku ya Bwana

5. Wakusujudie wote
Mbele ya kiti chako.
Zako, Bwana, nguvu zote
Itwae milki yako
Njoo Bwana,
Sisi tu watu wako.

Comments

Popular posts from this blog

52. Yote namtolea Yesu

85. Ni Mtu wa Simanzi

48. Naweka dhambi zangu